Friday, August 14, 2020

Dondoo za leo: Sugu asema ameachiwa na polisi bila chaji, Rais Magufuli ameagiza viongozi wa dini kuhamasisha kupiga kura na Chadema wataka uchunguzi waliochoma ofisi Arusha

 

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari leo Jumamosi ya Agosti 15, 2020.

Habari hizo ni Mgombea Ubunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi, asimulia jinsi polisi walivyowaachia bila chaji kulikoni?, Rais John Magufuli amewataka viongozi wa dini kuhamasisha kupiga kura na Chadema yataka uchunguzi waliochoma ofisi zao mkoani Arusha.

Karibu msomaji wetu;

SUGU: NIMEACHIWA NA POLISI BILA CHAJI NAJIULIZA NI KWELI WALITAKA KUPORA FOMU?

Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu amesema wamewekwa ndani kwa masaa matatu na kuachiwa bila chaji.

Sugu amesema amepandishwa karandinga na kuwekwa selo na wanambeya 15 akiwemo bibi wa miaka 70.

“Baada ya masaa matatu wametuachia bila chaji yoyote! Tunajiuliza what was the Motive? Ni kweli walitaka kupora fomu?,” alihoji sugu katika ukurasa wake wa twitter.

Soma zaidi

JPM: VIONGOZI WA DINI WAHAMASISHE KUPIGA KURA

RAIS John Magufuli amewataka viongozi wa dini kuhamasisha waumini wao kushiriki katika uchaguzi mkuu, hasa siku ya kupiga kura Oktoba 28, mwaka huu.

Kiongozi huyo wa nchi alitoa rai hiyo alipohutubia mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Kanisa la Asemblies of God (TAG) uliofanyika jijini hapa jana.

Alisema siku ya uchaguzi ni siku ya mapumziko na waendelee kumwomba Mungu wapatikane viongozi wenye maono.

“Wachapakazi na wazalendo kwa taifa letu, tusiangukie mikononi mwa viongozi wabadhirifu, wabinafsi au vibaraka maana kazi ya viongozi kama hao huwa ni kubomoa badala ya kujenga, kung’oa badala ya kupanda na kutawanya badala ya kukusanya,” alisema.

Soma zaidi

CHADEMA WATAKA UCHUNGUZI WALIOCHOMA OFISI ZAO ARUSHA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitaka serikali kuwakamata wahalifu waliochoma ofisi ya chama hicho Kanda ya Kaskazini.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, ofisi hizo zilizoko jijini Arusha, zilichomwa moto usiku wa kuamkia jana na kusababisha uharibifu wa samani zilizokuwamo na miundombinu ya jengo la ofisi hizo.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Benson Kagaila, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa, tukio hilo lilitokea majira ya kati ya saa nane na saa tisa usiku.

Kigaila alidai majirani wa ofisi hiyo walisikia kelele za mlinzi wa ofisi hizo akiomba msaada na baadaye sauti hiyo ilipotea.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/15/dondoo-za-leo-sugu-asema-ameachiwa-na-polisi-bila-chaji-rais-magufuli-ameagiza-viongozi-wa-dini-kuhamasisha-kupiga-kura-na-chadema-wataka-uchunguzi-waliochoma-ofisi-arusha/

No comments:

Post a Comment