Tuesday, August 11, 2020

Wanaume huangalia tabia kukatika ni mbwembwe tu upo hapo?

Habari ya muda huu wasomaji wetu. Nakukaribisha tena katika ukurasa wetu wa mahusiano.

Ukurasa huu ni kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya mahusiano ili tuweze kujifunza.

Leo tutajadili jambo hili kuna baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya ajabu ya kuzani kuwa wakiwakatikia wanaume wanapokuwa kitandani ndio kupendwa zaidi na mwanaume.

Hapa nataka tuelewane wapendwa kukatika kitandani sio kigezo cha mwanaume kukupenda upo hapo?

Mwanaume huangalia mambo mengi hasa mnapokuwa katika mahusiano ni vizuri ukaelewa vitu ambavyo mwanaume anapenda.

Unaweza ukawa unajitahidi kukatika kama feni lakini tabia yako ikawa ni mbaya kwa mwanaume wako.

Nataka nikuambia mwanaume huangalia mwanamke mwenye tabia nzuri sambamba na hekima yake huko kukatika ni chombeza tu.

Usije kujidanganya kumkatiakia mwanaume ndio kupendwa zaidi nataka nikuambia jurekebishe tabia yako iwe nzuri.

Wewe kila siku ni mgogoro ndani ya nyumba hakuna amani kila kukicha ni vurugu alafu unasema nikimkatikia mambo yataisa.

Nataka nikuambia mwanaume huwa anahesabu makosa tofauti na mwanamke na ikifika wakati akichola hata hajalishi viuno ulivyokuwa mnampa.

Kuna baadhi ya wanaume utasikia nampaka mauno mume wangu hawezi kuniacha nani kakuambia ukitoa mauno ndio huwezi kuachwa.

Acheni fikra hizo wanaume wanampenda mwanamke mwenye hekima zake anayejua maadili na pia awe na upeo wa maendeleo.

Hujawahi kusikia mwanaume akisema mwanamke wangu hata asipokatika kitandani siwezi kumuacha yule ni kichwa cha familia yangu.

Kwa hiyo katika mahusiano nataka nikuambie wanaume huangalia viti vingi acha kujidanganya kukatika ndio kupendwa.

Hivi kama hauna hata ushauri wa maendeleo kwa mumeo unazani utapendwa. Wewe kila siku ni kuwaza kuvaa nguo mpya na kuwaza mitoko.

Jifunze kuwa na hekima unapokuwa katika mahusiano hayo mengine ni chombeza tu.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/wanaume-huangalia-tabia-kukatika-ni-mbwebwe-tu-upo-hapo/

No comments:

Post a Comment