Saturday, August 15, 2020

Lema: Tume chukua hatua kwa vyombo vya ulinzi na usalama

Mgombea Ubunge jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, ameitaka Tume kuwachukulia hatua vyombo vyake ulinzi na usalama kwa kitendo cha kuchomwa ofisi.

“Tume wajue walio choma ofisi za Chadema Arusha moto, tume chukua hatua kwa vyombo vya ulinzi na Usalama,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa twitter.

“Nina matumaini makubwa kwamba hatua stahiki zitachukuliwa ili kuepusha chuki na visasi katika jamii,” aliandika Lema.

Lema alisema upumbavu kama huo ukifumbiwa macho ni hatari kwa nchi.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/15/lema-tume-chukua-hatua-kwa-vyombo-vya-ulinzi-na-usalama/

No comments:

Post a Comment