Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari leo Alhamisi ya Agosti 13, 2020.
Habari hizo ni Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) yatoa ufafanuzi kuhusiana na Tetemeko lililotokea jana katika baadhi ya mikoa na kuleta taharuki kwa wananchi, Mchungaji afikishwa mahakamani kwa madai ya kumbaka mwanafunzi je unajua ni wapi tukio hilo limetokea? na Vyama vya upinzani vimemjibu Mkuu wa jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kulikoni?
Karibu msomaji wetu;
TMA IMESEMA HAKUNA TISHIO LA TSUNAMI KUTOKANA NA TETEMEKO LILILOTOKEA JANA
Mamlaka ya hali ya hewa Tanazania (TMA), imesema hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko lililoteke jana kwa baadhi ya mikoa.
Jana saa 2:14 majira ya usiku limetokea tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha Ritcher 5.9 katika eneo la kusini Mashariki mwa mkoa wa Pwani katika bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA imeeleza wamefanya uchambuzi katika kituo chake cha tahadhari ya Tsunami ili kuona na kujiridhisha kwamba kuna uwezekano wowote wa tetemeko hilo kusababisha mawimbi ya Tsunami baharini.
MCHUNGAJI KORTINI MADAI KUBAKA MWANAFUNZI
MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chalinze, ambaye pia ni Mkuu wa Jimbo la Chalinze, Boniface Mgalula, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Lugoba mkoani Pwani akituhumiwa kumbaka mwanafunzi na kumpa mimba.
Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mwaria, Mwendesha Mashtaka, Zua Kawawa, alidai mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 6, mwaka huu .
Katika kesi namba 203 ya mwaka 2020 iliyosomwa mahakamani hapo Agost 11, mtuhumiwa alikana shtaka hilo na la kumtumia mwanafunzi huyo kuosha vyombo nyumbani kwake kama ilivyodaiwa na mwendesha mashtaka.
VYAMA VYA UPINZANI VYAMJIBU SIRRO
VYAMA vya siasa nchini vimeliomba Jeshi la Polisi kutenda haki na kutoonyesha kupendelea upande wowote kuelekea kwenye uchaguzi, ili kutunza amani na utulivu.
Kwa upande wake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, kwa kazi nzuri ya kulinda raia na mali zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao walisema iwapo jeshi hilo litasimamia sheria, kanuni na taratibu bila ubaguzi au kubeba chama chochote cha siasa, hakutakuwa na uvunjifu wa amani utakaotokea.
Viongozi hao walikuwa wakizungumzia kauli ya IGP Simon Sirro, aliyoitoa mwanzoni mwa wiki akihojiwa na Kituo cha luninga cha ITV, ambaye aliwaonya wanasiasa wanaoanzisha shari kupitia matamshi yao.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/dondoo-za-leo-tma-imesema-tetemeko-lililotokea-hakuna-tishio-la-tsunami-mchungaji-kortini-madai-kubaka-mwanafunzi-na-vyama-vya-upinzani-vyamjibu-sirro/
No comments:
Post a Comment