Thursday, August 13, 2020

Mwigulu Amlipua Zitto “Hamtarejesha hesabu ya fedha za mabwana  zenu”

Magufuli sacks Mwigulu Nchemba as Home Affairs Minister - The CitizenWaziri wa sheria na katiba Mwigulu Nchemba amemjibu kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe juu ya kauli yake aliyoitoa leo juu ya tume ya uchaguzi kutokuteua baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani kwenye nafasi za udiwani,ubunge na urais.

Mwigulu amejibu kauli ya Zitto kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa twiter na kuongeza kuwa tume itasimamia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba kwa sheria na kulinda amani ya nchi.

“Hautaharibika hata uchaguzi wa kata moja, tutasimamia sheria na tutalinda amani ya nchi yetu, hamtarejesha hesabu ya fedha za mabwana  zenu kwa damu za watoto wa watanzania” ameandika Mwigulu.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/mwigulu-amlipua-zitto-hamtarejesha-hesabu-ya-fedha-za-mabwana-zenu/

No comments:

Post a Comment