Monday, August 17, 2020

Mwanamke Mwenye Umri Mkubwa Zaidi Amerika Asherehekea Miaka 116 Kwa Njia ya Ajabu

Oldest black woman in US with 200 great grandchildren celebrates 116th birthday

Hester Ford, mwanamke raia wa Amerika anayedaiwa kuwa na umri mkubwa kuliko wote amewasha mtandao akisherehekea miaka 116 tangu kuzaliwa

Hester amebarikiwa na watoto 12 wajukuu 48 na vitukuu 200

Hester Ford rai wa Amerika mwenye umri mkubwa zaidi ameadhimisha siku ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 116 kwa njia ya kipekee.

Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, ajuza huyo ambaye ni mwenyeji wa Charlotte, North Carolina, alisherehekea siku ya kuzaliwa akiungana na baadhi ya wanafamilia yake.

Ford ambaye amebarikiwa na na watoto 12 wajukuu 48 na vitukuu 200 hakuweza kuandaa sherehe kubwa kufuatia kanuni za COVID19.

Ajuza huyo alizaliwa South Carolina 1904 kabla ya vita vya kwanza vya ulimwengu. Ford alipata umaarufu mkubwa Charlotte baada ya kuishi hapo kwa zaidi ya miaka 59.

Diwani wa Charlotte Vi Lyles alitenga Agosti 15 kama siku yake kama njia ya kumsherehekea na kusherehekea siku ya kuzaliwa.

La kushangaza ni kuwa ajuza huyo hana siri yoyote inayomfanya kuishi miaka mingi kiasi hicho huku rika zake wote wakiaga kitambo.

Ford alichukua usukani kama mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi Amerika baada ya Alelia Murphy kufariki 2019 akiwa na umri wa miaka 115.

Lucile Rando raia wa Paris ndiye anayedaiwa kuwa na umri mkubwa zaidi duaniani, akimpiku Ford kwa miezi saba.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/mwanamke-mwenye-umri-mkubwa-zaidi-amerika-asherehekea-miaka-116-kwa-njia-ya-ajabu/

No comments:

Post a Comment