Meneja wa kundi la WCB Sallam SK amesema kuwa alishindwa kumpa mkono wa salamu msanii Harmonize aliyekuwa kwenye kundi hilo wakati wa msiba wa mke wa meneja mwenza wa kundi hilo Hamis Tale (Babu Tale).
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na kituo cha televisheni cha Wasafi Sallam ameongeza kuwa amekuwa kwenye mgogoro na Harmonize kwa muda mrefu na alikuwa hasalimiani na msanii huyo kwa kipindi cha takribani miaka mitatu.
“Harmonize tumekaa miaka takribani minne hajawahi kunisalimia tangu akiwa WCB nilishawahi kukutana naye mara nyingi tu studio, benki hata uwanja wa ndege na akanipita bila hata kunisalimia kwa hiyo sikuona maan ya yeye kunisalimia tukiwa msibani” amesema Sallam.
Sallam ameongeza kuwa chanzo cha ugomvi baina yake na Harmonize ambaye kwa sasa ni msanii huru ni kitendo cha mkuu wa mkoa wa zamani wa Dar Es salaam Paul Makonda kumkaza msanii huyo juu ya uvutaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/sallam-afunguka-sababu-ya-kukataa-mkono-wa-harmonize/
No comments:
Post a Comment