Tuesday, August 11, 2020

Maamuzi ya Sakata la Morrison kufanyika kesho hali bado tete nyaraka yakosekana

Mwenyekiti wa kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Elias Mwanjala, amesema leo wameshindwa kufika maamuzi sakata la mkataba wa kati ya Bernard Morrison na Klabu ya Yanga.

Mwanjala alisema kuna nyaraka moja ambayo ni muhimu haijapatikana, hivyo wataendelea kesho na kikao chao.

“Kesi inaendelea leo tulitegemea kufanya maamuzi kwa bahati mbaya kuna taarifa muhimu haijakamilika tumehakikishiwa tunaipata kesho saa 2:30 asubuhi, ” alisema.

Alisema kesho saa nne asubuhi wataanza kikao na maamuzi yatatangazwa na Bonifance Wambua.

“Kuweni na subira mambo yanaenda vizuri tunasubiri document upande wa Morrison haujakamilika na upande wa Yanga,” alisema Mwanjala.

Hivi karibuni mchezaji Morrison ametimkia Klabu ya Simu huku Yanga wakidai hajamaliza mkataba aliopewa wa miaka miwili.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/maamuzi-ya-sakata-la-morrison-kufanyika-kesho-hali-bado-tete-nyaraka-yakosekana/

No comments:

Post a Comment