Saturday, August 15, 2020

Mkandarasi anayejenga barabara ya Sinza atakiwa kuikamisha haraka

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, amemuagiza Mkandarasi anayejenga barabara ya Shekilango Sinza kukamilisha ujenzi huo ifikapo Septemba 16 na endapo watakiuka makubaliano hayo Serikali itawatoza faini.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam, alipotembelea ujenzi wa barabara hiyo na daraja la mto Sinza na kukuta ujenzi wake ukiwa umefika asilimia 40 wakati lengo ni kukamilika mwezi ujao.

Amesema Serikali haitaongeza muda wa ziada wa kukamilisha mradi huo endapo Mkandarasi atashindwa kukamilisha mkataba wake kwa wakati.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/15/mkandarasi-anayejenga-barabara-ya-sinza-atakiwa-kuikamisha-haraka/

No comments:

Post a Comment