Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa mkuu wa mkoa wa Pwani na mkuu wa wilaya Mkuranga pamoja na mkurugenzi mtendaji wa halamshauri hiyo kuhakikisha shule za msingi na sekondari za mwarusembe zinapatiwa madawati.
Akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule hizo leo Agosti 13, 2020 amesema halmashauro hiyo inaviwanda vingi ni kitu cha kushangaza kuona wanafuzni wanakaa chini.
“Halmashauri yenu ina viwanda vingi kuliko wilaya zote, hivi vyote vinafanya nini? Kwa nini msiende kwenye viwanda vyenu mkaongee nao ili fedha ya CSR itumike kuondoa tatizo hili? Mapato yenu kwa mwaka ni zaidi ya shilingi bilioni mbili, zinafanya nini?” amesema Waziri Mkuu.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/majaliwa-atoa-wiki-moja-vigogo-mkoa-wa-pwani/
No comments:
Post a Comment