Wanaume hao, kila mmoja na mtoto mmoja
Mwanamke huyo amewapongeza pakubwa kwa kuishi naye kwa Amani
Kuishi kingi kuona mengi. Je umewahi kufiri kuhusu kisa ambako mwanamke anaolewa na wanaume wawili kisha wakaishi pamoja kwa amani?
Mwanamke mmoja raia wa Amerika amewasha mitandao na kuwaacha wengi vinywa wazi baada ya kubaini kuwa ameolewa na wanaume wawili. Si kuolewa tu, wanaume hao wanaishi naye katika chumba kimoja.
Mwanamke huyo aliyetambulika kama Kenya Stevens alichukua hatua ya kipekee kwa kupakia mtandaoni picha aliyopiga na wanaume wake hao wakiwa pamoja.
Kando na kuwasifia kwa kushi naye kwa amani, Kenya alijaribu kubainisha jinsi wachumba wake hao wanavyofanana.
‘’Hapa ni mimi na wapenzi wangu wa maisha. Wote wana urefu wa 6‘3. Wote wana ndevu. Sote tunatumia miwani. Tunaishi pamoja kwa amani. Nawalea wanao wa kiume- vijna hao wako shuleni.’’Kenya aliandika.
Kisa hiki kiliibua mjadala mitandaoni wengi wakidai kuwa wanaume hao wamerukwa akili.
Baadhi wakidai kuwa ni wanaume ambao hawataki majumu, na hivyo wanakaa na kulishwa kama wajinga, wengine nao wakieleza kuwa wamepumbazawa akili.
Msimamo wako ni upu?
Je, weweza kukubali kuolewa na wanaume wawili? Ama Je waweza kukubali kuoa mwanamke mmoja mkiwa wanaume wawili?
source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/kutana-na-wanaume-wawili-waliomuoa-mwanamke-mmoja-wanaishi-pamoja/
No comments:
Post a Comment