Tuesday, August 11, 2020

Kutana na Mapacha 3 wa Kike Waliofunga Harusi na Mapacha 3 wa Kiume

A collage of the triplets brothers and sisters on their wedding day. Photos source: Gistreel

Picha za harusi ya mapacha hao watatu wa kiume na wa kike. Picha: Hisani

Mapacha hao waliandaa sherehe ya harusi katika jimbo la Enugu Nigeria

Sherehe hiyo ya faragha ilhudhuriwa na waalikwa pekee

Picha za harusi ya mapacha hao watatu wa kiume na wa kike zimeibua mjadala mkubwa mitandaoni

Mitandao ya kijimaa iliwaka kwa ucheshi mkubwa huku picha za harusi za mapacha watatu wa kiume na kike zikisambaa kote.

Picha za mapacha hao wa kike wanaofanana kama shilingi kwa ya pili, Okwoma, Dumalu na Chinwe ziliwaacha wengi vinywa wazi haswa baada ya kubainika kuwa waliolewa na mapacha wengine watatu.

The Triplets walked down the aisle in grand style.Congratulations 🎤 to them…😍😍😍😍😍Chinedu Weds Dumalu, Chukwuebuka…

Posted by Diva Anita Brown on Sunday, 7 June 2020

Picha zao zilichapishwa katika mtandao wa facebook na mwanadada aliyetambulika kama Diva Anita Brown aliyekuchukua nafasi ya kipekee kuwapa heko kwa hatua walioichukua.

‘’ Mapacha hawa walifunga pingu za maisha kwa njia ya aina yake. Heko kwao. Chinedu amuoa Dumalu, Chukwuebuka amuoa Okwuoma na Kenechukwu amuoa Chinwe.  Tunasherehekea harusi ya mapacha hawa, pia ilete baraka kwetu sote.’’ Anita aliandika.

Sherehe ya harusi ya mapacha hao iliandaliwa faraghani, waalikwa pekee wakiruhusiwa kuhudhuria.

Mitandao iliwaka huku wengi wakiwarashia kwa jumbe za heri na pongezi na kuwatakia mema katika ndoa yao.

Kilichosalia kuwa swali kwa wengi ni kuhusu jinsi sita hao walivyokutana pamoja, wakapendana na kupanga kuoana.

Kweli hakuna kisichowezekana. Hapa Bongo Leo, tunawataki kilalaheri na baraka za ndoa.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/kutana-na-mapacha-3-wa-kike-waliofunga-harusi-na-mapacha-3-wa-kiume/

No comments:

Post a Comment