Rais wa nchi ya Urusi Vladimir Putin. Picha: Hisani
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameeleza kuwa wanasayansi wake wamefanikiwa kupata chanjo dhidi ya corona
Putin alitangaza Jumanne, Agosti 11 kuwa nchi yake ndiyo ya kwanza duniani kuidhinisha chanjo hiyo
Alieleza kuwa bintiye alikuwa kati ya watu waliopewa chanjo hiyo
Rais wa nchi ya Urusi Vladimir Putin ametangaza wazi kuwa nchi yake imefanikiwa kutengeneza na kuidhinisha chanjo ya virusi vya COVID19.
Akizungumza Jumanne, Agosti 11, Putin alibaini kuwa Urusi ndiyo nchini ya kwanza duniani kuweza kunda chanjo hiyo.
Kulingana na ripoti ya jarida la Washinton Post, Putin alitangaza kuwa bintiye alikuwa kati ya watu waliopata chanjo hiyo. Picha: Hisani
‘’ kilicho muhimu zaidi ni kuangazia ubora wa chanjo hiyo na matumizi yake siku za usoni,’’ alisema katika mkutano na maafisa wa serikali.
‘’Naamini kuwa hili litakamilika,’’ Putin aliongezea.
Kulingana na ripoti hiyo, watakaopewa kipau mbele katika chanjo hiyo ni wahudumu wa afya na walimu katika mwezi wa Agosti.
Hatua iliyochukuliwa na Urusi imeibua hisia, baadhi ya wansayansi duniani wakieleza kuwa chanjo hiyo huenda ikawa na madhara iwapo haitasubiri kujaribiwa na kuidhinishwa na rasmi nje ya nchi hiyo
Nchi zingine ambazo zipo mbioni kuunda chanjo ya COVID19 ni pamoja na Amerika, Uropa na Uchina.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/urusi-yatangulia-kuidhinisha-chanjo-ya-kwanza-ya-covid19-duniani/
No comments:
Post a Comment