Mlinzi wa ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini hajajulikana alipo baada ya ofisi kulipuliwa kwa petroli na kuteketea kwa moto.
Aliyekuwa Meya wa Ubungo, Bonifance Jacob amesema wanamuombea mlinzi wao aweze kupatikani akiwa mzima.
Jacob aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter huku akitoa pole kwa uongozi wa Chadema Arusha na Mwenyekiti wa Kanda Kaskazini, Godbless Lema kwa kuchomewa ofisi yao.
Usiku wa kuamkia leo ofisi hiyo imedaiwa kulipuliwa na petroli na watu wasiojulikana na kuteketea.
Natoa Pole Kwa Uongozi wa @CHADEMA Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa kanda ya Kaskazini @godbless_lema Kwa Kuchomewa Ofisi zao na Wapinzani wao Wakisiasa.
Naomba Mwenyezi Mungu asaidie Mlinzi aweze Kupatikana akiwa Mzima wa AfyaNAJUA CHADEMA KASKAZINI WANAJUA NINI CHA KUFANYA pic.twitter.com/ixWBXNbtvF
— Boniface Jacob (@MayorUbungo) August 14, 2020
Chadema imesema inaendelea na uchunguzi kubaini hatari zaidi inayoweza kuwa imewekwa.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/mlinzi-wa-ofisi-ya-chadema-iliyoteketea-kwa-moto-hajulikani-alipo/
No comments:
Post a Comment