Thursday, August 13, 2020

Jambazi Auawa Baada ya Kujeruhi Wananchi Wawili Kwa Risasi

Jambazi ataka fidia ya Sh270 milioni kwa kupigwa risasi akiiba ...Kamanda wa Polisi Mkoani wa Geita , ACP Mtatiro Kitinkwi amesema jeshi hilo limefanikiwa kumuua jambazi mmoja anayedaiwa kujeruhi wananchi wawili kwa risasi baada ya amjibizano na polisi.

Akizungumza na wanahabari mkoani ACP mtatiro amesema jambazi huyo aliyefahamika kwa jina la Daniel Jackson ameuawa baada ya kukaidi agizo la Polisi walipomtaka kujisalimisha.

“Baada ya jambazi huyo kuwaona Askari alikimbia huku akirusha risasi hovyo na kujeruhi raia wawili, Askari walimtaka ajisalimishe lakini akakaidi, na wao hawakumchelewesha wakampiga risasi”amenukuliwa acp Mtatiro.

Aidha, Jeshi hilo linashikilia bunduki yenye namba MV.97465X ambayo ilikuwa ikitumika katika tukio hilo la ujambazi.

CHANZO: JAMIIFORUMS

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/jambazi-auawa-baada-ya-kujeruhi-wananchi-wawili-kwa-risasi/

No comments:

Post a Comment