Monday, August 17, 2020

Yanga Kushusha Kocha Wiki Hii

Muwakilishi wa wadhamini wa klabu ya Yanga, mhandisi Hersi Said amesema klabu ya Yanga imeshapata kocha mkuu na kinachosubiria kwa sasa ni kukamilika kwa taratibu za kocha huyo kutua nchini kwani tayari anatoa maelekezo kwa timu kupitia kocha wa viungo anayesimamia maozezi ya timu hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa mjini Kinshansa alikokwenda kukutana na baadhi ya viongozi wa timu ya AS Vita, Hersi amesema timu inafanya mazoezi yote kwa malekezo ya mwalimu huyo na pengine wiki hii kocha huyo atawasili nchini.

“Kocha wetu yupo na anafanya kazi huko aliko anafanya kazi kwa njia ya simu anatuma ujumbe kwa kocha msaidizi na mazoezi yanaendelea kwa sasa kuna utaratibu wa usafiri na anaweza kuwsili nchini mapema  mwishoni mwa wiki hii na tutamtangaza kwa njia halali za klabu” amesema Hersi.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/yanga-kushusha-kocha-wiki-hii/

No comments:

Post a Comment