8Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania (TPBL) imetangaza rasmi ratiba ya msimu mpya wa ligi kuu bara unaotarajia kuanza mnamo September 6, 2020.
Mabingwa watetezi wa ligi bara Simba Sc watafungua pazia la ligi kuu bara dhidi ya Ihefu ya Mbeya siku ya Jumamosi September 6, 2020 wakati mabingwa wa Kihistoria wa ligi hiyo Yanga Wakicheza na Tanzania Prison kwenye uwanja wa Mkapa majira ya saa 1 usiku.
Mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utachezwa Oktoba 18 majira ya saa 11 jioni kwenye uwanja wa Mkapa.
Mechi zingine zitakazofungua ligi hiyo ni pamoja na Namungo Vs Coastal Unioni, Biashara Vs Gwambina, Dodoma Mji Vs Mwadui, Mtibwa Vs Ruvu Shooting, KMC vs Mbeya City, Kagera Sugar Vs JKT Tanzania na Azam Vs Polisi Tanzania.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/simba-vs-yanga-oktoba-81-ligi-kuanza-september-6/
No comments:
Post a Comment