Dada zake hao aliowatunga mimba wana umri wa miaka 17, 14 na 12 mtawalia. Picha: Hisani
Sampei Koisi alikamatwa na kufikishwa kortini kwa kuwatunga mimba dada zake
Mume huyo wa miaka 22 aliwatunga mimba dada hao wenye umri wa miaka 17, 16 na 12 baada kuwa na uhusiano wa kimahaba nao kwa miaka kadhaa
Wananchi wameiomba mahakama kutomuachilia kwa dhamana
Mitandao iliwaka moto baada ya habari kufichuka kuhusu jamaa aliyewatunga mimba dada zake watatu wenye umri mdogo.
Kulingana na kisa hicho kilichopeperushwa katika runinga ya Citizen, Jumatatu, Agosti 10, Sampei Koisi mwenye umri wa miaka 22 anadaiwa kuwatunga mimba dada zake watatu baada ya kulala nao kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Sampei atazuilia kwa muda zaidi huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kisa hicho. Picha: Hisani
Dada zake hao aliowatunga mimba wana umri wa miaka 17, 14 na 12 mtawalia.
Alizungumza katika Mahakama ya Kajiado, Sampei alikiri kufanya kitendo hicho, lakini akakana baadaye, baada ya kusomewa mashtaka kwa lugha ya nyumbani.
Hakimu katika Mahakama hiyo alitoa agizo ya kumzuilia kwa muda zaidi huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kisa hicho.
Wanamtandao pia waliiomba mahakama hiyo isimuachilie kwa dhamana wakidai kuwa angemtunga mimba mwengine tena.
Visa vya watoto wa shule kupata uja uzito tangu kulipuka kwa virusi vya corona vimeongezeka maradufu, serikali ikiwaomba wazazi kuwapa wanao mwongozo mwema.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/kisa-cha-jamaa-aliyewatunga-mimba-dada-zake-watatu-chini-ya-mwaka-moja/
No comments:
Post a Comment