Tuesday, August 25, 2020

Dondoo za leo; Mdee amkwepa Gwajima, Aporwa fomu, Vita CHADEMA, NCCR furaha CCM

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Mdee kumkwepa Gwajima, Aporwa fomu na vita ya CHADEMA, NCCR furaha ya CCM, kivipi? Karibu

MDEE GWAJIMA KITU GANI?

HALIMA Mdee, Mgombea Ubunge Kawe, Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema ‘Gwajima (Josephat Gwajima) kitu gani.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam.

Amesema, kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, katika Jimbo la Kawe alilokuwa akiliongoza kwa miaka kumi mfululizo, mshindi atatokana na mkakati wake kwa wapiga kura.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020, muda mfupi baada ya kurudisha fomu ya uteuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea jimbo hilo na kukidhi masharti ya ujazaji wa fomu ya uteuzi.

Soma zaidi>>>

MGOMBEA APORWA FOMU

MGOMBEA ubunge wa Morogoro Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abeid Mlapakolo, amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa kufanikisha kupatikana kwa fomu zake za kugombea ubunge wa jimbo hilo zilizokuwa zimeporwa na watu wasiojulikana.

Mlapakolo alisema tukio la kuvamiwa na kuporwa fomu hizo lilitokea jana asubuhi wakati akienda kwenye ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo kutekeleza matakwa ya sheria za uchaguzi kurejesha fomu kabla ya saa 10.

Soma zaidi>>>

VITA CHADEMA, NCCR FURAHA CCM

TANGU kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi, mkoa wa Kilimanjaro umekuwa ngome ya upinzani kwa kupitia vyama vya NCCR Mageuzi na Chadema, ambavyo vimetoa wakati mgumu kwa CCM kujinafasi katika majimbo tisa ya mkoa huo.

Awali NCCR Mageuzi ilishika hatamu katika mkoa huo kutokana na umaarufu wa aliyekuwa mgombea urais mwaka 1995, Agustine Mrema (Vunjo).

Ilhali baadaye Chadema nayo ilijimwambafai baada ya kuuweka kando ufalme wa NCCR Mageuzi kwa kupitia Freeman Mbowe (Hai) ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/08/26/dondoo-za-leo-mdee-amkwepa-gwajima-aporwa-fomu-vita-chadema-nccr-furaha-ccm/

No comments:

Post a Comment