Waziri Mkuu Hassan Diab aliongoza katika kujiuzulu Jumatatu, Agosti 10
Rais Michel Aoun alimuomba Diab kushikilia wadhifa huo kabla kufanyika uteuzi mwingine
Diab amechukua hatua ya kujiuzulu kufuatia maandano makali ya wananchi baada ya mlipuko wa Beirut
Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab alichukua nafasi ya kipekee Jumatatu, Agosti 10 kutangaza kuhusu kujiuzulu kwa serikali yake nzima.
Diab alichukua hatua hiyo wiki moja tu baada ya mlipuko wa ajabu katika mji mkuu wa Beirut uluowaua zaidi ya watu 150, kuwajeruhi maelfu na kuwaacha wengi bila makazi.
Rais Michel Auon alimuomba Diab kushikilia nafasi hiyo kama kaimu hadi wakati serikali nyingine inapoteuliwa kuchukua hatamu. Picha: Hisani
Diab aliamua kujiuzulu pamoja na serikali yake nzima huku maandamano yakishika kasi nchini humo, wananchi wakikabiliana na maafisa wa polisi katika mvutano mkali.
Licha ya kukubali hatua hiyo ya kujiuzulu, Rais Michel Auon wa nchi hiyo alimuomba Diab kushikilia nafasi hiyo kama kaimu hadi wakati serikali nyingine inapoteuliwa kuchukua hatamu.
Kujiuzulu kwa serikali hiyo kunajiri wakati mataifa mbali mbali yakiongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron akiandaa mkutano wa kimtandao na kuahidi TSh 600 bilioni kuisaidia nchi hiyo.
Kupitia kwa waziri wa mambo ya nje, Jean-Yves Le Drian, Rais huyo aliiomba serikali ya Lebanon kuhakikisha kuwa msaada huo unakwenda moja kwa moja kwa wananchi.
Rais wa Amerika Donald Trump pia aliahidi kutuma msaada wake kwa serikali hiyo.
Je, waunga mkono hatua ya kujiuzulu kwa serikali ya Lebanon?
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/serikali-ya-lebanon-yajiuzuli-kufuatia-mlipuku-wa-beirut-habari-kamili/
No comments:
Post a Comment