Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.
Zinazobamba leo ni pamoja na nyomi la CHADEMA lazua jambo, wahujumu waonywa na mwisho ni juu ya NEC kutangza wabunge wateule 18. Karibu;
UMATI WA CHADEMA WAZUA JAMBO
Utata mkubwa umeibuka juu ya picha zilizosambazwa mitandaoni juu ya watu waliohudhuria ufunguzi wa kampeni za mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Ndugu Tundu Antipas Lissu siku ya jana kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem
Hii ni moja ya picha za juu iliyopingwa kwenye mkutano huo siku ya jana na kupostiwa katika mtandao wa Instagram kwenye akaunti maalumu ya TBC .
Watu mbalimbali walionekana kuwa na mtizamo tofauti na badhi yao wakidai kuwa picha hiyo ilipingwa wakati wa mchana pale ambapo mgombea urais wa chama hicho alikua hajapanda jukwaani na wengine wakidai kuwa ilikua jioni.
Hisia mbalimbali zimeibuka juu ya picha hizi na wengi wakiziangalia kama kupungua kwa ushawishi wa Chama hicho kikuu cha upinzani nchini
Soma zaidi>>>
WAHUJUMU CCM WAONYWA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara, kimewatahadharisha baadhi ya viongozi wa chama wanaofanya vikao usiku vya kukihujumu chama hicho.
Kimeonya na kusema hakitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kufanya vikao vyao bila kuwa na vibali.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Ghaib Lingo, alitoa tahadhari hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea wateule wa ubunge na udiwani uliofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Kijiji cha Endasak.
Soma zaidi>>>
NEC YATANGAZA WAMBUNGE WATEULE 18
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza wabunge wateule 18 wa chama tawa cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania ambao wanasubiri kuapishwa.
Taarifa ya Mkurugenzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera ambayo ameitoa jana usiku Ijumaa tarehe 28 Agosti 2020 imesema, wateule hao wamepatikana baada ya wagombea wenzao kujikuta wanapoteza sifa na kubaki peke yao.
Majimbo hayo 18 ni kati ya 264 ambayo yanafanya Uchaguzi Mkuu Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020 na tayari kampeni za uchaguzi huo zimekwisha kuanza.
Soma zaidi>>>
source http://www.bongoleo.com/2020/08/29/dondoo-za-leo-utata-nyomi-la-uzinduzi-kampeni-chadema-wapanga-usiku-kucha-kuihujumu-ccm-nec-yatangaza-wabunge-wateule18/
No comments:
Post a Comment