Karibuni kwenye safu yetu ya mahusiano nimekuja na mambo motomoto naomba ukae mkaa wa kupokea na kiyafanyia kazi.
Leo nipo na wale wanawake wanaolea tabia ya uvivu wa kudamka kitandani, wakimuacha mume akiamka na kujiandalia kila kitu.
Najua imeanza kukuingia akilini! Hivi nikuulize mwanamke mwenzangu huoni aibu mume kukuacha kitandani kisha akajihudumia kila kitu mwenyewe wakati wewe ni mzima na huna tatizo lolote?
Wanawake wa siku hizi ndoa zinatushinda kwa sababu tunapenda kushindana na wanaume, eti akikwambia mke wangu kaniwekee maji ya kuoga, unamwambia umechoka, jana umelala saa sita, hivi unadhani ni sawa sawa.
Nakukumbusha, kitanda ulikiacha kwenu na kama unaweza kuiheshimu ofisi ukaamka mapema kuikimbilia, hivi unashindwa nini kuamka mapema kwa ajili ya mumeo?
Ndoa inatafutwa upo? nakusihi sana ulikumbuke hilo kabla ya kuja kujuta baadaye, maana ukishaachwa utaanza kumtafuta mchawi wakati umejiroga mwenyewe.
Wanawake wenzangu niwakumbushe tu kitu kidogo, raha ya mapenzi ni kudamka asikwambie mtu, Mume ni kama mtoto mchanga, anahitaji malezi hivyo ni jukumu lako kudamka asubuhi na mapema kabla yeye hajatoka kitandani ili umuandae vizuri hata kama haendi kazini.
Hivi mumeo kaamka, kaenda zake kaoga kaingia jikoni kajitengenezea chai, unapoamka unamkuta akinywa huku anatazama televisheni sebuleni, unajisikiaje? Halafu anakuuliza leo tutakula nini? Wakati muda huo wewe hata mswaki hujapiga mtoto wa kike, hivi na akili zako utalijibu swali hilo?
Embu jirekebisheni wanawake wenzangu kuna mambo mengine mnalazimisha wanaume wenu kutenda dhambi.
Kuna vitu vidogo mnasababisha wanaume wawatafutie mchepuko ndipo akili itakukaa sawa. Hivi kweli unashindwa kuamka mapema na kumuandaa mume wako.
Yule ndio kama mtoto wako ambaye unamuandaa aende shule, hivyo amka asubuhi na kumuandaa acha uvivu wa kijinga.
Hakuna kitu mwanaume anachopenda kama kuandaliwa asubuhi na unahakikisha anaenda kazini akiwa mtanashati
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/wanawake-acheni-uvivu-kuamka-asubuhi-raha-ya-penzi-ujue-kumuandaa-mpenzi-wako/
No comments:
Post a Comment