Wednesday, August 12, 2020

Mkurugenzi Aliyedanganya Gari ya Wagonjwa Asamehewa

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Rufiji Kamishna Msaidizi Onesmo Lyanga amesema kuwa Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa kaimu mkurugezi wa Halmashauri hiyo Brighton Kilimba baada ya kutoa taarifa za uongo kuhusu gari la wagonjwa.

Akinukuliwa na kituo cha habari cha ITV Kamishna Onesmo amesema msamaha huo umetoka leo na mkurugebzi huyo yupo huru licha taratibu za kumpeleka mahakamani kuwa zilikwisha kamilika.

Mapema Julai 30 mwaka huu majira ya saa 9 mchana Rais Magufuli akitokea  kijijini Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara katika maziko ya aliyekuwa  rais wa awamu ya tatu aliposimama Ikwiriri Rufiji mkoani Pwani kusikikiza  kero mbalimbali inadaiwa Bw. Kilimba  alitoa  taarifa  za uongo  kwa Mhe  rais kuwa  gari  la kubebea wagonjwa ni bovu  liko gereji na linahitaji gharama kubwa za matengenezo  wakati  anajua sio kweli.

 

CHANZO: ITV

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/mkurugenzi-aliyedanganya-gari-ya-wagonjwa-asamehewa/

No comments:

Post a Comment