Mke alianza kumuonyesha madharau siku ya harusi, alikataa kuoiga picha naye. Picha: Hisani
Humphrey Kiama alieleza jinsi mpenziwe alivyotema siku ya harusi na kumuendea mume mwengine
Baada ya kumtema, mwanadada huyo alianza kueneza uvumi kuwa aliamuacha maana hana uwezo wa kuzalisha
Kiama alioa mke mwengine na kujaliwa watoto wanne
Maisha ya ndoa ni kama trapeziamu, yana pande nyingi, ukiwa upande huu unaweza kukosa kujua yaliyoko upande ule mwingine.
Jamaa mmoja aliyetambulika kama Humphrey Kiama amekumbuka aibu aliyopata baada ya kumpenda kipusa mmoja na kupiga hatua ya kupanga harusi naye baada ya muda wa uhusiano.
Kulingana na Kiama, mke alianza kumuonyesha madharau siku ya harusi, akifika kiwango cha kukataa kupiga picha naye hata mbele ya mchungaji aliyekuwa akiwaunganisha.
‘’Baada ya kula kiapo, tulipiga magoti kufanyiwa maombi. Nilikuwa nimemshika mkono, ghafla akaurusha mkono wangu. Hata alikataa kupiga picha nami.’’ Kiama alisema.
Licha ya changamoto hizo, Kiama aliamua kutunza ndoa baada ya kuchukua kiapo akijua fika kuwa ndoa ya harusi huhitai uvumilivu.
Kiama aliendelea kusimulia kwa uchungu, usiku huo, rafiki yao mmoja tajiri aliwaandalia karamu katika eneo la Kiserian, na hapo ndipo bibi harusi alivyomtema hadharani.
‘’ Jamaa mmoja tajiri alituandalia sherehe eneo la Kiserian. Wakati wa sherehe hiyo, bibi yangu alianiacha na kuenda kustarehe na mume mwengine. Niliona aibu. Tulipofika nyumbani, tulizozana sana, Baada ya mwezi moja tuliachana,’’ aliongezea.
Kiama ambaye sasa amejaliwa watoto wanne na mwanamke aliyemuoa baadaye ameeleza kuwa bibi harusi huyo alianza kueneza uwongo kuwa alimuacha kwa kuwa gumba.
‘’Baada ya kuachana, alisambaza ujumbe kuwa mimi ni gumba. Ningepita mahali ama hata kwa daladala na watu wananiangalia visivyo. Nilikuwa na uchungu mwingi. Singeweza kulia. Niliweza kuoa baadaye na sasa nina watoto wanne, watatu wa kiume na mmoja wa kike.’’ Alisimulia.
Ingekuwa ni wewe, ungefanyaje?
source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/jamaa-asimulia-jinsi-mkewe-alivyomtema-hadharani-siku-ya-harusi/
No comments:
Post a Comment