Friday, August 14, 2020

‘’Hata Kwa Nyani Hatutumii’ Amerika Yatofautiana na Urusi Kuhusu Chanjo ya COVID19

Putin invited Donald Trump to Moscow in weekend call, Kremlin says ...

Rais Trump alipashwa habari kuhusu chanjo ya serikali ya Putin. Picha: Hisani.

Serikali ya Amerika ilieleza kuwa haitakubali chanjo hiyo kutoka Urusi

Mamlaka ya Urusi imedai kuwa Amerika itazidi kubaki kunyuma kwa kutoamini Urusi

Urusi imeeleza kuwa hiyo ndiyo sababu Amerika imekataa chanjo yao

Serikali ya Urusi imetangaza kuwa tayari kushirikiana na Amerika ili kusaidia katika kubuni chanjo ya COVID19. Hii ni siku chache tu baada ya nchi hiyo kuthibitisha kubuni na kuidhinisha matumizi ya chanjo yao.

Aidha, Urusi imedai kuwa Amerika haipo tayari kupata usaidizi wao.

Kulingana na ripoti jarida la CNN, serikali ya Urusi imedai kuwa Amerika itasalia kuwa nyuma katika masuala mengi kwa kukosa kuamini Urusi.

‘’ Kuna vile Amerika imekosa uaminifu na Urusi,’’ afisa huyo alinukuliwa.

‘’ Tunaamini kuwa teknolojia ya Urusi kuhusu kubuni chanjo, majaribio na matumizi hayakubaliki huku kwa kukosa uaminifu,’’ aliongezea.

Aidha, ripoti hiyo ilibaini kuwa Rais Donald Trump alikuwa amejuzwa kuhusu chanjo hiyo ya Urusi.

Katibu katika Idara ya mawasiliano ya ikulu hiyo Kayleigh McEnany akisema kuwa chanjo za Amerika hupitia majaribio makali katika viwango vitatu.

Maafisa wengine wa serikali ya Amerika wameilaumu Urusi wakidai kuwa chanjo yao haijafikia viwango vifaavyo kuruhusiwa kwa matumizi kwa wanadamu.

‘’Amerika haiwezi kujaribu chanji ya Urusi hata kwa nyani,’’ Afisa mmoja wa afya alisema.

Rais Putin wa Urusi amesisitiza kuwa chanjo yake  ya COVID19 ipo shawari na wanaoipinga ni propaganda tu. Hii ni baada ya rais huyo kubaini kuwa bintiye ni kati ya watu wa kwanza waliopewa chanjo hiyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/hata-kwa-nyani-hatutumii-amerika-yatofautiana-na-urusi-kuhusu-chanjo-ya-covid19/

No comments:

Post a Comment