Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa haujaridhishwa na maamuzi ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji juu ya kesi baina ya klabu hiyo na mchezaji Bernard Morrison.
Katika taarifa ikiyotolewa na klabu hiyo imesema kuwa inatarajia kukata rufaa kwenye mahakama ya rufaa ya maswala ya soka (CAS).
Taarifa ya Yanga imesema kuwa wanasubiri nakara ya hukumu kutoka kwenye kamati hiyo kisha kwenda CAS kutafuta haki.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/baada-ya-kushindwa-yanga-kukata-rufaa-cas/
No comments:
Post a Comment