Mgombea urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amewataka viongozi wa dini mbalimbali nchini wanaoshiriki kwenye mkutano wa kamati ya taifa ya amani kutowasahau baadhi ya viongozi wa dini waliopo magerezani na wanaotoa vitisho vya uraia vya viongozi wenzao.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Tundu Lissu ametuma ujumbe wa kuwataka viongozi hao wa dini kukumbuka juu ya masheikh wa uamsho walioko gerezani tangu mwaka 2014 na kuwataka kutafakari waraka wa kwaresma wa maaskofu wa TEC na KKKT.
“Viongozi wa dini msiwasahau Masheikh wa Uamsho walioko gerezani tangu 2014. Kumbukeni mashtaka dhidi ya Askofu Gwajima na vitisho vya uraia wa Maaskofu Niwemugizi na Kakobe na Padre Ray Saba. Na tafakarini Waraka wa Kwaresma wa Maaskofu wa TEC na KKKT 2017” amendika Lissu.
Ujumbe wa Lissu unakuja saa kadha kabla ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua rasmi mkutano wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu na kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.
Viongozi wa dini msiwasahau Masheikh wa Uamsho walioko gerezani tangu 2014. Kumbukeni mashtaka dhidi ya Askofu Gwajima na vitisho vya uraia wa Maaskofu Niwemugizi na Kakobe na Padre Ray Saba. Na tafakarini Waraka wa Kwaresma wa Maaskofu wa TEC na KKKT 2017. #SASABASI #Niyeye2020 pic.twitter.com/lWLQQBOvrf
— Tundu Antiphas Lissu (@TunduALissu) August 17, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/lissu-atuma-ujumbe-mzito-kwa-vingozi-wa-dini/
No comments:
Post a Comment