Lionel Messi. Picha: Hisani
Messi analalia godoro la £900 kumkinga dhidi ya kuambukizwa covid19
Godoro hilo hundoa chembe chembe zote za virusi vya corona chini ya saa nne
Saul Niguez, Sergio Aguero pia ni mabalozo wa kampuni ya kuunda godoro hilo
Baada ya muda wa kutoa ufadhili kwa umma katika kupambana na virusi vya corona, nyota wa Barcelona Lionel Messi sasa amechukua hatua ya kujikinga na kuikinga familia yake dhidi ya virusi hivyo hatari.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 anadaiwa kununua godoro la TSh 3 Milioni lenye uwezo wa kuondoa viiini vinayoambukiza virusi vya corona kwa zaidi ya 99%.
Tec Moon ni mojawapo ya kampuni zinazounda magodoro ghali zaidi duniani, sasa ikibainika kuwa kampuni hiyo umeunda godoro maalum lenye uwezo wa kuondoa bakteria. Lionel Messi akiwa kati watu wa kwanza kuweza kulinunua.
Godoro hilo lina uwezo wa kuikanda miguu. Picha: Hisani.
Nyota wa Atletico Madrid Saul Niguez pamoja na Sergio Aguero ni kati ya mabalozo wa kampuni hiyo maarufu.
Kando na kulalia, godoro hilo lina uwezo wa kuikanda miguu, na kuizuia dhizi ya kuokota virusi.
Kando na kujilinda dhidi ya virusi hivyo, Messi ameendelea kutoa msaada kwa mji wake, Rosario, Argentina.
Hadi sasa, nyota huyo ametoa takriban vipumuzi 50 kusaidia katika kuwaokoa walioathirika na virusi hivyo.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/lionel-messi-anunua-godoro-la-tsh-3-milioni-kujikinga-dhidi-ya-covid19/
No comments:
Post a Comment