Sunday, August 30, 2020

Dondoo za leo; Siku 100 za Lissu Ikulu, Aaaga dunia kwa kulipukiwa bomu, UVCCM wamvaa

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na NA SIKU 100 ZA Lissu ikulu, alipukiwa na bomu na mwisho ni juu ya UVCCM kumvaa Maalaim Seif

SIKU 100 ZA LISSU

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Tundu Antipas Lissu katika muendelezo wa kampeni zake jijini Dar es salaam ambapo leo Agosti 30 zimefanyika katika viwanja vya Liwiti Tabata amesema Nchi inahitaji maridhiano ya kitaifa.

Amesema katika siku 100 za kwanza baada ya kupata ushindi katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28, ataunda tume kwa ajili ya upatanishi na ukweli ili kuvumbua mabaya yanayofanyika katika nchi.

ALIPUKIWA BOMU

Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama amesema,

”Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras  mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota Bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kuripuka na kusababisha apoteze maisha”.

Soma zaidi>>>

UVCCM WAMVAA

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umelaani kauli zinazodaiwa kutolewa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kwa mujibu wa UVCCM, kauli hizo zinaashiria uvunjifu wa amani wakati huu wakati huu wa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ; na zimekiuka  tamko la vyama vya siasa la kuendesha kampeni za kistaarabu.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Mussa Haji Mussa aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa kauli zilizotolewa na mgombea huyo, zina lengo la kuwatia hofu wananchi wasijitokeze kupiga kura na hazikubaliki.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/31/dondoo-za-leo-siku-100-za-lissu-ikulu-aaaga-dunia-kwa-kulipukiwa-bomu-uvccm-wamvaa/

No comments:

Post a Comment