Monday, August 31, 2020

Dondoo za leo; Membe na kinachoiua CCM,CCM yataka asiwataje, Manzese kula ubwabwa wa Rungwe jumamosi

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo na Membe ataja kinachoiua CCM, CCM yataka wasiwataje ana mwisho ni juu ya Rungwe kuzindua kampeni zake jumamosi hii.

KINACHOIUA CCM

BERNARD Membe, mgomeba urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ametaja kitachoiua Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Amesema, sumu kubwa iliyopandwa na chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, ni mpasuko ndani ya chama hicho.

Membe ametoa kauli hiyo jana Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 katika uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya ACT-Wazalendo, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Membe aliyekuwa waziti wa mambo ya nje kuanzia mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawal wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kiwkete amesema, ndani ya CCM kuna mpasuko baina ya kundi la wanachama wapya na wa zamani.

Soma zaidi>>>

CCM YATAKA ASIWATAJE

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetuma salamu kwa vyama vya upinzani kwa kuwataka kuacha chokochoko na wasioutakia mema nchi yetu huku kikitoa rai kwa wapinzani kuacha kutaja taja majina ya viongozi wao.

Akizungumza leo jijini Dodoma ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphery Polepole amesema kabla ya kusoma majina ya wagombea waliopitishwa kugombea ujumbe w baraza la wawakilishi ni vema kwanza akazungumzia mwenendo wa kampeni unavyoendelea kule Zanzibar na siasa zake.

Hivyo amesema kwamba “tungependa kuujulisha umma ya kwamba Chama Cha Mapinduzi tuko vizuri mno kwa maana ya wana CCM kule , wananchi wa kawaida kule, ambao wanatuelewa vizuri mno , wameupokea vizuri zaidi uteuzi wa ndugu yetu Hussein Mwinyi ambaye mpaka sasa hivi tumesema usikimbie.

UBWABWA WA RUNGWE JUMAMOSI

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Chaumma, Hashimu Rungwe, ametangaza kuzindua kampeni zake za urais wa chama hicho Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 Manzese jijini Dar es Salaam.

“Chaumma itaongea na wananchi 5 Septemba 2020 katika Uwanja wa Manzese Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana. Wananchi waje wasikilize, tunachowaambia. Wakija pale watapata kila kitu na watauliza maswali na tutawajibu.Wako watu wenye hamu ya ubwabwa waje tutajua tunawapatiaje,” amesema Rungwe



source http://www.bongoleo.com/2020/09/01/dondoo-za-leo-membe-na-kinachoiua-ccmccm-yataka-asiwataje-manzese-kula-ubwabwa-wa-rungwe-jumamosi/

No comments:

Post a Comment