Thursday, August 13, 2020

Heche aicharua Takukuru kuwaachia CCM waliowakamata kwa rushwa

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amehoji Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iweje waliokamatwa kwa rushwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuachiwa.

Alisema Takukuru iliwahoji wabunge wa Chadema kwa tuhuma za watu waliohama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Leo mliodai kuwakamata na rushwa CCM mmeamua kuwaachia CCM wenyewe? Au CCM ina Takukuru yake binafsi,” aliandika Heche katika ukurasa wake wa twitter

Aliandika ujumbe unaosome hivi “Takukuru mnachekesha sana yaani wabunge wa Chadema mliwahoji kwa tuhuma za watu waliohama Chadema!!! Leo mliodai kuwakamata na rushwa CCM mmeamua kuwaachia CCM wenyewe? Au CCM ina Takukuru binafsi..,”.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/heche-aicharua-takukuru-kuwaachia-ccm-waliowakamata-kwa-rushwa/

No comments:

Post a Comment