Mwenyekiti wa kamati ya hadhi ya wachezaji wa shirikisho la soka la nchini (TFF) Elias Mwanjala ameamua kuwa mchezaji Bernad Morrison kuwa mchezaji huru na kamati hiyo haitambu mkataba wa miaka miwili ulisaini mchezaji huyo.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam amesema mkataba baina ya Morrison na Yanga ulikuwa na mapungufu kadhaa yaliyopelekea uamuzi huo wa kumpa Morrison kama mchezaji huru.
“Ni mchezaji huru kutokana na mkataba wake kuwa na matatizo kidogo, mkataba uliokuwepo ulitakiwa kuisha tarehe 14 March, huku mkataba wa pili ulioletwa kwetu ukionyesha umesainiwa mwezi saba pia baadhi ya kursa kutokuwa na saini ya mchezaji na mtu mwingine kama shahidi kinachofuatiwa kwa sasa amepekewa kwenye kamati ya maadili” amesema Mwanjala.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/morrison-aishinda-yanga-tff/
No comments:
Post a Comment