Thursday, August 13, 2020

Dondoo za leo: Ofisi ya Chadema yalipuliwa kwa Petroli na kuteketea, Mahakama yamuamuru Lissu kufika mahakamani na Heche aicharua Takukuru kuiachia CCM waliowakamata kwa rushwa

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari leo Ijumaa ya Agosti 14, 2020.

Habari hizo ni Ofisi ya Chadema yalipuliwa kwa Petroli na kuteketea je unajua ni wapi?, Mahakama imeagiza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu lissu kufika mahakamani kulikoni? na Aliyekuwa mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amewatolea povu Takukuru kuwaachia CCM waliowakamata kwa rushwa.

Katibu msomaji wetu

OFISI YA CHADEMA YALIPULIWA KWA PETROLI NA KUTEKETEA

Ofisi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Kaskazini imechomwa moto na kuteketea usiku wa kuamkia leo mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo ameitoa Aliyekuwa mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kupitia ukurasa wake wa twitter.

“Ofisi yetu ya @Chademakaskazini imechomwa moto na kuteketea yote usiku wa kuamkia leo,” aliandika Mdee

Soma zaidi

MAHAKAMA YAMWAMURU LISSU KUFIKA MAHAKAMANI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwamuru kufika mahakamani mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake watatu, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, Septemba 14, mwaka huu, baada ya jana kushindwa kufika kusikiliza kesi yake.

Amri hiyo ilitolewa jana na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai shauri lilipangwa kwa kutajwa na kwamba mshtakiwa Lissu, hakufika kusikiliza kesi yake.

Mdhamini wa Lissu, Robert Katula, alidai mshtakiwa aliwasiliana naye juzi asubuhi na kumueleza kwamba yuko mkoani anatafuta wadhamini kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.

Soma zaidi

HECHE AICHARUA TAKUKURU KUWAACHIA CCM WALIOWAKAMATA KWA RUSHWA

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amehoji Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iweje waliokamatwa kwa rushwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuachiwa.

Alisema Takukuru iliwahoji wabunge wa Chadema kwa tuhuma za watu waliohama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Leo mliodai kuwakamata na rushwa CCM mmeamua kuwaachia CCM wenyewe? Au CCM ina Takukuru yake binafsi,” aliandika Heche katika ukurasa wake wa twitter

Soma zaidi



source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/dondoo-za-leo-ofisi-ya-chadema-yalipuliwa-kwa-petroli-na-kuteketea-mahakama-yamuamuru-lissu-kufika-mahakamani-na-heche-aicharua-takukuru-kuiachia-ccm-waliowakamata-kwa-rushwa/

No comments:

Post a Comment