Rais John Magufuli amefanya mabadiliko kwa wakuu wa wilaya leo kwa kuwahamisha vituo vyao vya kazi.
Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Simon Kemori Chacha, kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Didoma, Simon Ezekiel Odunga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Mabadiliko ya vituo vya kazi kwa wakuu wa wilaya hao yanaanza leo Agosti 13, 2020.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/rais-magufuli-amefanya-mabadiliko-kwa-wakuu-wa-wilaya-wawili/
No comments:
Post a Comment