Wednesday, August 12, 2020

Mwanamke Akiri Kuwaambukiza Wengi Virusi Vya Ukimwi Makusudi, Afunguka Kuhusu Chanzo

Image

Harriet akiri kuwaambukiza wanaume virusi vya HIV makusudi. Picha: Hisani

Alikiri kuwaambukiza wanaume wengi virusi vya HIV makusudi

Alidai kuwa alichukua hatua hiyo kutokana na uchungu aliokuwa nao

Ameomba msamaha na kuwataka wote aliolala nao kufanya vipimo vya HIV

Mwanadada mmoja mwenye urembo wa kupindukia amejitokea wazi na kutangaza kuwa aliwaambukiza wanaume wengi virusi hatari vya HIV makusudi.

Kipusa huyo anayetambulika katika mtandao wa Instagram kama ‘akunavaharriet’ alikiri kupitia kwa ukurasa wake kuwa aliamua kuwaambukiza wengi virusi hivyo kutokana na uchungu aliokuwa nao.

‘’Wakati umefika kujitokeza wazi, nimekuwa na machungu kwa miezi lakini sasa siwezi kuendelea nao tena. Nina virusi vya HIV na nimekuwa nikiwaambukiza wanaume, poleni, mniwie radhi, iwapo nililala nawe, enda ukafanyiwe vipimo. Harriet aliandika.

Kando na kuandika, Hariet alipiga hatua zaidi na kupakia video mtandaini kuthibitisha  matokeo ya vipimo vilivyoonyesha ameambukizwa virusi hivyo.

Mitandao imewaka moto Harriet akishambuliwa kwa kuamua kuangamiza wengine licha ya kujua wazi kuwa anaugua.

Aidha, wameitaka serikali kumchukulia hatua za kisheria kwa kuwaangamiza wengine kwa maradhi hayo makusudi.

Kulingana na sheria, ni hatia kumuambukiza mtu yeyote virusi kama hivyo makusudi, yeyote anayepatikana kufanya hilo hupata adhabu ya kifungo cha miaka 15 gerezani ama hata kifungo cha maisha.

Iwapo Harriet atapatikana na hatia, huenda akapata adhabu mojawapo.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/mwanamke-akiri-kuwaambukiza-wengi-virusi-vya-ukimwi-makusudi-afunguka-kuhusu-chanzo/

No comments:

Post a Comment