Thursday, August 13, 2020

Takukuru yawafikisha mahakamani watu watatu akiwemo Diwani wa CCM

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma imewafikisha mahakamani Diwani wa kata ya Ntyuka, Theobald Maina (44), Benedict Mazengo (60) ambaye ni Afisa mtendaji, na Anderson Jonathan aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Chimala kwa kujipatia Sh milioni 2 kwa njia za udanganyifu.

Mkuu wa Takukuru Dodoma, Sosthenes Kibwengo akizungumza na waandishi wa habari leo alisema viongozi hao watatu wanashtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya mamlaka kinyume cha sheria.

Alisema uchunguzi umeonyesha Aprili 2016 watuhumiwa kwa pamoja walitumia vibaya madaraka yao na hivyo kujipatia kwa njia kughushi shilingi milioni mbili ambazo ni malipo ya minara ya simu iliopo kwenye Kata ya Ntyuka.

Alisema watuhumiwa walifuja fedha hizo badala ya kusimamia ili zitumike kwa ajili ya kununua vifaa vya Ujenzi wa ofisi ya mtaa wa Ntyuka.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/takukuru-yawafikisha-mahakamani-watu-watatu-akiwemo-diwani-wa-ccm/

No comments:

Post a Comment