Monday, August 17, 2020

Kisa cha Mwanamke Aliyeachiliwa Kuenda Nyumbani Licha ya Kupatikana na COVID19 Mara 3 Chini ya Siku 32

Coronavirus disease (COVID-19)

Jerotich Seii alienda karantini Julai baada ya kupatikana na virusi vya corona

Hii ni baada ya kuonyesha dalili za virusi hivyo

Licha ya kupna kutokaka na dalili za virusi, alipatikana na virusi hivyo baada ya vipimo

Mtetezi wa haki za kibanadumu maarufu nchini Kenya Jerotich Seii amethibitisha kuwa amepewa idhini ya kutoka karantini licha ya kupimwa na kupatikana na virusi vya corona.

Jerotich ambaye alitiwa karantini nyumbani kwake kwa siku 32 alieleza kuwa madaktari walimfanyia vipimo mara tatu kwa muda huo za vyote vikaonyesha anauagua COVID19.

‘’ Vipimo kwa mara ya tatu jana. Siku 32 tangu nilipotiwa karantini bado vinaonyesha nina virusi vya corona. Nini hii?  Daktari wangu aliangalia hali yangu na kulingana na kanuni za CDC, naweza kusema sina COVID19, niko huru kuondoka karantini,’’’ alisema.

Mtetezi huyo wa haki za kibiadamu alieleza kuwa dalili zote za virusi vya corona vimetoweka.

Alipotiwa karantini na kuanza matibabu, alikuwa na maumivu ya viongo, shida ya kupumua, kikohozi, maumivu ya kichwa na hata akakosa hamu ya chakula.

‘’ Ingawa si kawaida, haijawahi kutokea mtu kupimwa na kupatikana na COVID19 mfululizo haswa wale wenye dalili za ugonjwa huo. Mimi ni mmoja wao. Huenda nilikuwa na virusi kupita kiasi na hivyo inachukua muda kutoweka kabisa mwilini,’’ aliongezea.

Jerotich alishangaa kuhusu kupatikana na virusi hivyo mara tatu hata baada ya kupona kabisa.

Kenya imezidi kurekodi visa vya maambukizi na idadi kubwa ya wanaopona haswa hutoka katika karantini za nyumbani. Hadi sasa, jumla ya waliopona wakiwa 15,970.

Tanzania haijarekodi maambukizi yoyote ya COVID19 tangu Mei, 2020.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/kisa-cha-mwanamke-aliyeachiliwa-kuenda-nyumbani-licha-ya-kupatikana-na-covid19-mara-3-chini-ya-siku-32/

No comments:

Post a Comment