Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari leo Agosti 11, 2020.
Habari hizo ni Kauli ya IGP Sirro kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu je unajua ni kipi alichokisema? Sophia Simba apeta ubunge CCM na Sakata la mchezaji Marrison na Yanga kujulikana leo mapema.
Karibu msomaji wetu;
KAULI YA IGP KWA LISSU
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Simon Sirro, amewaonya wanasiasa walioanza kuonyesha shari kupitia matamshi na sura zao kuelekea uchaguzi mkuu.
Sirro pia amezungumzia maendeleo ya uchunguzi wa jeshi hilo kuhusu shambulio la kupigwa risasi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.
IGP Sirro alizungumzia masuala hayo juzi wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV.
Kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi aliwataka wanasiasa kutolichokoza jeshi hilo na pia wasililaumu litakapochukua hatua dhidi yao.
“Nimeona viongozi wa siasa wanazungumza mambo makali sana. Ninawaheshimu viongozi wote wa siasa katika ngazi zote lakini lazima sheria na kanuni zilizopo ziheshimiwe.
SOPHIA SIMBA APETA UBUNGE CCM
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM aliyefukuzwa uanachama na baadaye kurejea tena, Sophia Simba, ameonyesha kurejea tena katika duru za siasa nchini baada ya kupenya kwenye tatu bora za kuwania ubunge wa viti maalum.
Juzi, Sophia katika kura za maoni za kuwasaka wabunge wa viti maalum kuwakilisha taasisi zisizo za kiserikali (NGOs), alishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 43.
Kundi hilo lilikuwa na wagombea 21 na nafasi zilizokuwa zikiwaniwa ni tatu, Neema Lugangila akiongoza kwa kura 60 akifuatwa na aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Rita Mlaki, aliyepata kura 48.
SAKATA LA MORRISON NA YANGA KUJULIKANA LEO
Mwenyekiti wa kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Elias Mwanjala, amesema leo watatoa maamuzi katika mkataba wa mchezaji Bernard Morrison na Klabu ya Yanga.
Akuzungumza na waandishi wa habari jana amesema wameshindwa kufika maamuzi jana kwa sababu kuna vitu muhimu vimekosekana.
Mwanjala alisema kuna nyaraka moja ambayo ni muhimu haijapatikana, hivyo wataendelea leo na kikao chao.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/dondoo-a-leo-kauli-ya-igp-kwa-lissu-sophia-simba-apeta-ubunge-ccm-na-sakata-la-morrison-na-yanga-kujulikana-leo/
No comments:
Post a Comment