Monday, August 24, 2020

Dondoo za leo; Dk. Shika afariki, Lissu aibua hofu mpya, Chadema yatoa onyo kwa wasaliti

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Dr. Shika kufariki dunia, hofu yata nda Chadema juu ya Lissu,  na mwisho ni juu ya Chadema kuwaonya wasaliti, kulikoni? Karibu

DR SHIKA AFARIKI DUNIA

Dr Louis Shika maarufu kama Mzee wa 900 Itapendeza amefariki dunia, akiwa nyumbani kwa kaka yake wakati wa uangalizi baada ya matibabu katika Hospital ya Nyanguge iliyopo Wilayani Magu nje kidogo ya Jiji la Mwanza.

Awali Dr Shika Aalikuwa amelazwa Hospitali hapo kwa muda mrefu akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya figo.

Global Publishers tumezungumza na daktari kutoka Hospitalini hapo ambaye allikuwa akimtibu na kuthibitisha kuwa Dr Shika amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Soma zaidi>>>

TUNDU LISSU AIBUA HOFU

HOFU mpya imeanza kutanda nchini Tanzania juu ya hatma ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kufuatia madai kuwa aweza kuenguliwa kugombea nafasi hiyo. Anaripoti Saed Kubenea…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Chadema, hofu ya kuenguliwa kwa Lissu inatokana na kuzagaa mitandaoni, kwa madai kuwa kuna mpango wa kumuengua mwanasiasa huyo, kwa kutumia sababu mbalimbali za kisheria, ikiwamo makosa ya kimaadili na kuanza kampeni mapema.

Hata hivyo, Lissu mwenyewe, amewahi kujibu madai hayo mara kwa mara akisema, anachofanya sio kuanza kampeni kabla ya wakati, na kwamba hakuna sheria yeyote inayozua mtu kuanza kampeni kabla ya muda uliowekwa.

Soma zaidi>>>

CHADEMA YAWAONYA WASALITI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Victoria inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, Zacharia Obad ametoa onyo kwa wanachama wa chama hicho waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali kutoleta visingizio ili wajitoe kushiriki uchaguzi Mkuu kwani kufanya hivyo ni usaliti kwa Chama.

Alitoa onyo hilo wakati akizungumuza na wanachama waliopitishwa kuwania nafasi za udiwani na ubunge mkoani Mwanza ambapo alisisitiza hawategemei kuona hujuma ya aina yeyote kutoka kwa watu walioaminiwa na chama hicho, kwani chama kimefanya uwekezaji mkubwa kuanzia mchakato wa kura za maoni mpaka kuelekea kampeni zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/08/25/dondoo-za-leo-dk-shika-afariki-lissu-aibua-hofu-mpya-chadema-yatoa-onyo-kwa-wasaliti/

No comments:

Post a Comment