Serikali ya jimbo la Lagos ilitoa idhini ya kufunguliwa makanisa tena
Kibali hicho kilitolewa licha ya idadi ya maambukizi ya COVID19 kupanda
Makanisa ya wachungaji hao maarufu yamesalia mahame, ibada zikifanyika mitandaoni
Tunde Bakare, Pasta Sam Adeyemi na Prophet TB Joshua ni wachungaji maarufu wa Nigeria waliokataa kufungua tena makanisa yao licha ya serikali kusitisha marufuku hiyo.
Kila mmoja wao alitoa sababu ya kuwafanya kutofungua makanisa hayo.
- Prophet TB Joshua
Kiongozi huyo wa makanisa ya SCOAN alieleza kuwa hatafungua makanisa yake hadi pale Mungu anapozunguza naye kuhusu kufanya hivyo.
- Pasta Sam Adeyami
Pasta Sam Adeyami. Picha: Hisani
Mchungaji huyo alieleza kuwa kanisa lake halitafungua hadi pale hali ya kawaida itakaporejea. Kulingana naye, hataki kuhatarisha maisha ya waumini.
Pasta Tunde Bakari
Kiongozi huyo wa makanisa ya Citadel Gloval Community (CGCC) alishangaa ni kwanini serikali iliamua kusitisha marufuku ya kufunguliwa makanisa huku maambukizi ya Corona yakifika kileleni.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesisitiza kuwa wanasayansi wake wamebuni chanjo ya COVID19 na tayari imeidhinishwa kwa matumizi, mwanawe wa kike akiwa kati ya watu wa kwanza waliopewa chanjo hiyo.
Licha ya maambukizi hayo kuteketeza kote duniani na katika mataifa jirani, Tanzania, serikali ya Tanzania kupitia kwa Ras Magufuli amesisitiza kuwa maradhi hayo hayapo nchini.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/wachungaji-maarufu-wa-nigeria-wadinda-kufungua-makanisa-licha-ya-serikali-kutoa-marufuku-uhondo-kamili/
No comments:
Post a Comment