Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera amesaini mkataba wa kufundisha klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda kucheza ligi kuu kuanzia msimu ujao.
Zahera aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instragram majira ya usiku kuwa anarudi Tanzania kuungana na timu ya Gwambina ambayo itacheza ligi Kuu Tanzania bara Agosti 21, 2020.
Novemba 5, 2017 Klabu ya Yanga ilivunja mkataba wa Zahera pamoja na benchi nzima la ufundi sambamba na kuvunja kamati ya mashindano.
Zahera aliiongoza Klabu ya Yanga kwa miezi 15 akichukua nafasi ya ya Mzambia, George Lwandamina.
Kocha Mkuu wa zamani wa club ya Yanga SC Mwinyi Zahera usiku huu ametangazwa kupitia kurasa za instagram za Gwambina FC ya Misungwi Mwanza kuwa ameungana nao, Zahera anarudi Tanzania kuungana na Gwambina timu ambayo itacheza Ligi Kuu Tazania bara 2020/21 #MillardAyoSPORTS pic.twitter.com/dcDN4FSiI5
— millardayo (@millardayo) August 10, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/zahera-kurejea-nchini-asaini-mkataba/
No comments:
Post a Comment