Wednesday, August 12, 2020

Morrison Amkurupua Roma “Mbona Anakuja Kimgogoro Mgogoro”

Mwanamuziki Roma ambaye pia ni shabiki wa klabu ya simba amehoji kama winga mpya wa klabu hiyo Bernard Morrison amekuja na baraka kwenye klabu hiyo kutokana na kitendo cha usajili wake kugubikwa na mizegwe ya kesi tokakwenye klabu yake ya zamani.

Roma ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa kitendo cha kushinda kwa mchezaji huyo nisawa lakini anachokiona kama kuna watu hawajakunjua nafsi winge huyo kutua msimbazi.

“Ni Sawa Ameshinda, Lakini Mbona Morrison Mwenyewe Anakuja Kimgogoro Mgogoro Hivi? Yani Kama Kuna Watu Hawajakunjua Hivi Nafsi Zao!! Kweli Atakuwa Na Baraka Zote Huyu?  Inanichanganya Sana Hii Situation!!” ameandika Roma.

Mapema leo Agosti 12, 2020 mwenyekiti wa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji Elias Mwanjala ametangza kuwa mchezaji huyo ameshinda kesi yake ya kimkataba baina yake na Yanga mabo imedumu kwa siku tatu ndani ya kamati hiyo.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/morrison-amkurupua-roma-mbona-anakuja-kimgogoro-mgogoro/

No comments:

Post a Comment