Sunday, August 16, 2020

Nape: Uchaguzi ukiisha tabu inabaki kwa wapambe ambao leo wanakesha karibu kuchomoka roho

Mgombea ubunge jimbo la Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema  uchaguzi unapomalizika wakubwa hukutana na kumaliza tabu inabaki kwa wapambe.

Nape ameandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa twitter kuwa “Naangalia makamiano kuelekea uchaguzi wa Oktoba 28 … kwa hulka ya wanasiasa uchaguzi ukiisha wakubwa hukaa na kumaliza, tabu hubaki kwa wapambe sasa ambao leo wanakesha karibu kuchomoka roho,”

“Kuna maisha baada ya uchaguzi , penda na chukia kwa kiasi, ” aliandika Nape



source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/nape-uchaguzi-ukiisha-tabu-inabaki-kwa-wapambe-ambao-leo-wanakesha-karibu-kuchomoka-roho/

No comments:

Post a Comment