Sheikh Hamdan bin Mohammed bin Rashid Al Maktoum aliacha gari lake aina ya Mercedes-Benz G Wagon kwa ndege wake wawili kutagia na kuangulia mayai
Katika video iliyosambaa mitandaoni, ndege hao wanaonekana wakijenga viota
Sheikh ameeleza kuwa alichukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa ndege hao hawatatizwi wanapotaga
Mwana wa mfalme wa Dubai, Sheikh Hamdan bin Mohammed bin Rashid Al Maktoum amewasha mitandao kwa hatua aliyoichukua kuhakikisha kuwa ndege wake wawili wanatunzwa kifahari.
Rashid aliwaacha wengi vinywa wazi baada ya kubaini kuwa aliwaachia ndege wake wawili gari lake la kifahri aina ya Mercedes-Benz G Wagon kujengea viota na kutagia mayai.
Kulingana naye, aliacha kulitumia gari hilo kuhakikisha kuwa ndege hao wanataga bila kutatizwa.
Katika video ambayo imesambaa mitandaoni, ndege wawili wanaonekana wakijenga viota kwenye gari hilo.
Kando na huyo, ndege mwengine anaonekana akiwa anaangua mayai yake.
Video: Sheikh @HamdanMohammed won't use his SUV for a while, and here's why https://t.co/yVhQ22Bz0j#Dubai pic.twitter.com/TLCbPx1WTo
— Khaleej Times (@khaleejtimes) August 4, 2020
Si hayo tu, gari hilo wanakotagia na kuangulia mayai limezingirwa na kamba nyekundu kuashiria kuwa yeyote hahitajiki eneo hilo.
Video hiyo iliibua mdahalo mkubwa mtandaoni wengi wakishangaa ni kwanini tajiri huyo alichukua hatua hiyo badala ya kutumia hela hizo kuwasaidia wasiojiweza, wengine wakimuunga mkono kwa kuwatunza ndege wake kifahari
Je wewe umefanya nini kumtunza huyo mnyama unayemfuga?
source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/mwana-wa-mfalme-wa-dubai-atoa-gari-la-tsh-30-milioni-kwa-ndege-kujengea-viota/
No comments:
Post a Comment