Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amewataka wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini kukutana ofisini kwa akili ya kumpokea, Tundu Lissu.
Lema aliandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa twitter akiwataka wanachama hao kukutana katika ofisi ya chama Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya kumpokea mgombea urais Lissu.
Lissu anawasili leo mkoani Arusha kwa akili ya kutafuta wadhamani.
Ofisi hiyo usiku wa kuamkia leo imelipuliwa kwa petroli na watu wasiojulikana na kuteketea kwa moto.
WANACHAMA WETU WOTE WA CHAMA MKOA ARUSHA NA KANDA YA KASKAZINI TUKUTANE OFISI YA CHAMA KANDA YA KASKAZINI SAA TATU NA NUSU TUKAMPOMKEE MGOMBEA URAIS WETU MH TUNDU LISSU .
— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) August 14, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/lema-tukutane-ofisi-ya-kanda-kaskazini-tukampokee-lissu/
No comments:
Post a Comment