Wednesday, August 26, 2020

Dondoo za leo: Mapingamizi ya Lissu kwa JPM, Lipumba yatupwa, awekwa mbaroni kwa utekaji, Vyombo vya habari vyaonywa

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na mapingamizi ya Lissu kutupwa, Mbaraoni kwa utekaaji wa  mgombea na mwisho ni juu ya

NEC NA LISSU

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeyatupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema dhidi ya wagombea wenzake wawili katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.

Lissu aliwawekea pingamizi jana Jumatano tarehe 26 Agosti 2020, Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Miongoni mwa sababu alizoeleza Lissu zilizomfanya kuweka pingamizi ni makosa yaliyomo kwenye fomu za Rais Magufuli na Profesa Lipumba ikiwemo Rais Magufuli kuwasilisha picha zisizo sahihi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera amesema, baada ya kupokea mapingamizi aliwajulisha wahusika ambao walitoa utetezi wao.

Soma zaidi>>>

MBARONI KWA UTEKAJI

MTU mmoja (jina linahifadhiwa) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kuhusika kumteka nyara mgombea udiwani kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Kerege Wilaya ya Bagamoyo, Martine Sultan.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 22, mwaka huu, katka Kitongoji cha Manofu, Kerege ambapo watu wanne wanaodaiwa kuwa wanaume, walimteka mgombea huyo.

Wankyo alisema baada ya jeshi hilo kupata taarifa, walifuatilia na kumkamata mmoja wa watuhumiwa hao akiwa katika Kijiji cha Janga, Mlandizi wilayani Kibaha.

Soma zaidi>>>

VYOMBO VYA HABARI VYAONYWA

Siku moja baada ya kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea wa kiti cha Urais,makamu wa rais, wabunge na madiwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetoa angalizo kwa vyombo vya Habari kutotangaza majina ya wagombea waliopita bila kupingwa kabla ya tume kuwatangaza kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kusababisha vurugu.

Wakati zoezi la uteuzi wa wakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa wanawania nafasi za udiwani, ubunge Urais na makamu wa Rais likikamilika NEC inatoa angalizo hilo kufuatia baadhi ya vyombo vya Habari kuwatangaza wagombea hao jambo ambalo ni kinyume na sheria ya uchaguzi.

Soma zaidi>>>

Tukimalizia dondoo hebu tuangazie jambo hili la mdau anayeomba ushauri jinsi ya kuishi na Boyfriend wake mchafu;

Kuna mdau anaomba msaada wa namna ya kuishi na Mwanaume yaani ‘Boyfriend’ wake asiye na tabia ya usafi kuanzia mwilini hadi mahali anapokaa (ndani kwake)

Mdau anasema “Mimi sio mtu msafi sana ila Mwanaume huyu amenishinda. Ni mtu mzuri na nimekuwa naye kwa miezi 8 sasa, mwanzo sikuwa nimemuelewa ila huyu Mwanaume ni mchafu sana.”

Anaendelea “Akioga usiku kabla ya kulala asubuhi haogi. Yaani analala na Mwanamke usiku, asubuhi anaenda kazini hivyo hivyo. Hata nikisema hasikii wala haelewi, ndio kwanza anasema nampanda kichwani.”

Aidha, amesema “Chumba chake ndo kichafu usiseme. Kuna wakati nilisafiri kama mwezi hivi kurudi chumba hakitamaniki. Nikamsafishia na kila weekend nikawa naenda kusafisha. Nilipata ugeni na sikwenda kwake kama wiki mbili, nilivyoenda nilikuta sahani alizolia chakula siku kama 3 zilizopita zipo humo, machupa ya maji, maganda ya ndizi”

Mdau anaomba maoni yenu amfanye nini boyfriend wake aache hiyo tabia na je, anaweza kuishi naye vipi?



source http://www.bongoleo.com/2020/08/27/dondoo-za-leo-mapingamizi-ya-lissu-kwa-jpm-lipumba-yatupwa-awekwa-mbaroni-kwa-utekaji-vyombo-vya-habari-vyaonywa/

No comments:

Post a Comment