Monday, August 17, 2020

Nyota wa Man United Paul Scholes Amuanika Mchezaji Aliyewauza Dhidi ya Savilla

A tribute to young Paul Scholes (he scores goals) at Manchester ...

Paul Scholes amemlaumu Lindelof kwa kuacha mianya katika kiungo cha ulinzi na kuipa Sevilla nafasi ya kuwanyuka bao la ushindi

Luul de Jong alimcheza difenda huyo wa Uswidi na kufunga bao la ushindi kunako dakika ya 78

Bruno alifungia Man United bao la ufunguzi dakika chache kabla ya Suso kusawazisha muda mfupi baadaye

Klabu ya Man United imetemwa nje ya ligi ya Uropa baada ya kuonyeshwa adabu na klabu ya Sevilla Jumapili, Agoti 16.

Timu  hiyo sasa imemlaumu pakubwa Lindelof wa kiungo cha ulinzi kufuatia masaibu ya timu hiyo.

Nyota wa timu hiyo Paul Scholes sasa anadai kuwa Lindelof anapaswa kubadilishwa ili asicheze katika timu ya kwanza wa klabu hiyo.

Victor Lindelöf - Player profile 19/20 | Transfermarkt

Scholes amemtaka Lindelof kutolewa katika timu ya kwanza ya Man United. Picha: Hisani.

Man United ilichukua uongozi wa mapema kupitia kwa mshabulizi Bruno Fernandes  kwa bao la kwanza kabla ya mahasimu Savilla kuokoa na kuwapiga bao la ushindi kunako dakika la 78.

Luuk de Jong alizitikisa nyavu kwa bao la ushindi baada ya kumsoma na kumcheza Lindelof na kuutumia mwanya huo ufaavyo.

‘’ Unaweza kulaumu kiungo cha ulinzi chote kwa kufuatia bao hilo.  Williams hafikii mpira huku Magure ni,  sijui. Lakini shida kuu ni Lindelof,’’ Scholes aliliambia BT Sport.

 

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/17/nyota-wa-man-united-paul-scholes-amuanika-mchezaji-aliyewauza-dhidi-ya-savilla/

No comments:

Post a Comment