Ikiwa zimepita dakika kadhaa baada ya mwenyekiti wa kamati ya maadili na hadhi za wachezaji wa shirikisho la soka nchini (TFF) Elius Mwanjala kutangaza kuwa mchezaji Bernard Morrison ameshinda kesi yake dhidi ya klabu yake ya zamani Yanga.
Klabu iliyomtanza hivi karibuni Simba SC imetuma ujumbe wa kumtambulisha rasmi Morrison kama mchezaji halari wa timu hiyo baada ya kumalizika kwa kesi hiyo.
“Morrison ni mnyama Karibu sana Msimbazi Bernard Morrison” umesomeka ujumbe uliotumwa kwenye ukurasa rasmi wa simba kwenye mitandao ya kijamii ikimatanishwa na video ya Bernard Morrison aikiwaomba mashabiki wa simba kumpokea.
MORRISON NI MNYAMA
Karibu sana Msimbazi Bernard Morrison (@Bm3Morrison) #MorrisonIsRed #NguvuMoja pic.twitter.com/xfpYxFvieQ
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) August 12, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/08/12/walichosema-simba-baada-ya-morrison-kuwashinda-yanga/
No comments:
Post a Comment