Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema kuna watu wanatoa rushwa jambo ambalo limekatazwa kwenye sheria ya gharama za uchaguzi.
“Hii ni rushwa ya uchaguzi, tendon lililokatazwa chini ya sheria ya gharama za uchaguzi,” aliandika Lissu katika ukurasa wake wa twitter.
“Popote atakapogombea awekewe pingamizi na mgombea wetu ili aenguliwe kwa mujibu wa sheria,”
Lissu ambaye ni mgombea Urais amesema watoa rushwa hao wafuatiliwe kila mahali waliko na kuwekewa mapingamizi ili uteuzi wao utenguliwe.
Hii ni rushwa ya uchaguzi, tendo lililokatazwa chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi. Popote atakapogombea awekewe pingamizi na mgombea wetu ili aenguliwe kwa mujibu wa sheria. Watoa rushwa hawa wafuatiliwe kila mahali waliko na kuwekewa mapingamizi ili uteuzi wao utenguliwe. pic.twitter.com/63TiH1DAWR
— Tundu Antiphas Lissu (@TunduALissu) August 13, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/08/13/lissu-atema-cheche-wagombea-wanaotoa-rushwa-ataka-wachukuliwe-hatua/
No comments:
Post a Comment