Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema wananchi wa kijiji cha Nanjilinji wamelalamikia kutolipwa fedha zao za mazao.
Zitto aliandika ujumbe huo katika akaunti yake ya Twitter kuwa jana jioni alizungumza na wananchi wa kijiji hicho na kuanza kulalamikia fedha zao katika zao la ufuta.
“Katika hii huzalisha zaidi ya tani 4,000 za ufuta kwa mwaka wenye thamani ya zaidi ya sh bilioni kwa mwaka,” aliandika Zitto.
Leo jioni nimezungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nanjilinji ambao malalamiko yao makubwa ni kutolipwa Fedha zao kwa wakati mara wauzapo mazao yao hasa Ufuta. Kata hii huzalisha zaidi ya tani 4,000 za Ufuta kwa mwaka wenye thamani ya zaidi ya Shs Bilioni kwa Mwaka. pic.twitter.com/QgOZARJskE
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) August 10, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/08/11/zitto-wananchi-wanalalamikia-malipo-yao-kwenye-zao-la-ufuta/
No comments:
Post a Comment